Luke 6:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo mfurahi na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu mna thawabu kuu mbinguni. Baba zao waliwafanyia manabii vivyo hivyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Furahini na kurukaruka kwa shangwe kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Furahieni siku ile na kurukaruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Furahini siku ile na kurukaruka! Kwani tazameni, mshahara wenu ni mwingi mbinguni! Kwani hivyo ndivyo, baba zao walivyowafanyia wafumbuaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Furahiwani siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mambo hayo yatakapotokea, mufurahi na kurukaruka, maana munawekewa zawadi kubwa mbinguni. Ni hivi babu zao walivyowatendea manabii.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Furahini siku ile, mkaruke: kwa kuwa bakika thawabu yenu nyiugi mbinguni, maana baba zao waliwatenda manabii mambo kama hayo.