Luke 6:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyanganya koti lako mwachie pia shati lako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu akikupiga shavu moja, mwache akupige na la pili pia. Mtu akichukua koti lako, usimkataze kuchukua shati pia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako mwachie pia shati lako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako mwachie pia shati lako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili. Mtu akikunyang'anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyang’anya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang'anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyanganya koti lako mwachie pia shati lako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akikupiga kofi shavu moja, umgeuzie la pili, alipige nalo! Mtu anayekunyang'anya kanzu yako, usimkataze kuichukua hata shuka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama mutu akikupiga kofi kwa shavu moja, umugeuzie lingine vilevile. Kama mutu akikunyanganya koti yako, umwachie shemizi yako vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akupigae shavu moja, umgeuzie la pili, nae akunyangʼanyae joho yako usimzuilie na kanzu.