Luke 6:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, msifiwe kwa sababu ya kuwapenda wale wanaowapenda ninyi tu? Hapana, hata wenye dhambi, wanawapenda wale wanaowapenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda ninyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwapenda wale wawapendao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana mkiwapenda wanaowapendani mnawagawia nini? Kwani nao wakosaji huwapenda wawapendao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonyesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Muko na shukrani gani kama munawapenda tu wale wanaowapenda? Kwa maana hata wenye zambi wanawapenda wale wanaowapenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi mkiwajienda wao wawapendao ninyi mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi huwapenda wao wawapendao.