Luke 6:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, msifiwe kwa kuwa mnawatendea mema wale wanaowatendea mema ninyi? Hapana, hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ hufanya vivyo hivyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ hufanya vivyo hivyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mnapowafanyia mema wanaowafanyia mema ninyi mnawagawia nini? Nao wakosaji hufanya hivyo hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muko na shukrani gani kama munawatendea mema tu wale wanaowatendea mema? Hata wenye zambi wanafanya hivi vilevile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mkiwatenda mema wao wawatendao ninyi mema, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.