Luke 6:34 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Je, msifiwe kwa kuwa mnawakopesha watu kwa kutarajia kupata vitu kutoka kwao? Hapana, hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wengine, ili warudishiwe kiasi kile kile!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwakopesha wenye dhambi wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwakopesha ‘wenye dhambi’ wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nanyi mnapokopesha watu, mnaowangojea kurudishiwa nao, mnawagawia nini? Nao wakosaji huwakopesha wakosaji wenzao, warudishiwe yaleyale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonyesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, muko na shukrani gani kama munawakopesha tu wale munaowatumainia kwamba watawarudishia? Hata wenye zambi wanawakopesha wenye zambi wenzao kusudi warudishiwe tena mali ile ile!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mkikopesha watu mkitumaini kupata kitu kwao tena, mna neema gani? Maana hatta wenye dhambi hukopesha wenye dhambi, illi wapokee sawasawa.