Luke 6:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Haikuruhusiwa mtu kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daudi alikwenda katika nyumba ya Mungu, akachukua mikate iliyotolewa kwa Mungu na kuila. Na kuwapa wenzake baadhi ya mikate hiyo. Hii ilikuwa kinyume na Sheria ya Musa, inayosema kuwa makuhani pekee ndiyo wanaoruhusiwa kula mikate hiyo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Kisheria, ni makuhani tu peke yao ndio walioruhusiwa kula mikate hiyo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Haikuruhusiwa mtu kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua ile mikate mitakatifu ambayo huliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake wakala!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya wonesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye aliingia katika nyumba ya Mungu, akachukua ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu, akala na kuwapa wenzake. Haikuruhusiwa mtu kula mikate hiyo isipokuwa tu makuhani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu, akaitwaa mikate aliyowekewa Bwana, akaila, akawapa nao wenziwe. Nayo kuila ni mwiko, huliwa na watambikaji peke yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya Wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akakamata mikate mitakatifu iliyotolewa kwa Mungu, akaikula na kuwapa watu wake vilevile, ijapokuwa mikate ile iliruhusiwa kukuliwa na makuhani wenyewe tu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate iliyotolewa kwa Mungu, akaila, akawapa na hawo waliokuwa pamoja nae, isiyo halali kuliwa illa na makuhani peke yao?