Luke 6:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Unawezaje kumwambia rafiki yako, ‘Hebu nikitoe kipande cha vumbi kilicho katika jicho lako’? Je, huwezi kukiona kipande cha ubao kilicho katika jicho lako mwenyewe? Wewe ni mnafiki. Kwanza kitoe kipande cha ubao katika jicho lako, ndipo utaona vyema na utaweza kukitoa kipande cha vumbi kilicho katika jicho la rafiki yako.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Au, unawezaje kumwambia mwenzako, Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi katika jicho lako, na huku huioni boriti iliyoko katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyoko jichoni mwako, na hivyo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, niache nikitoe hicho kibanzi kilichoko ndani ya jicho lako’, wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyoko ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa kwanza boriti ndani ya jicho lako, ndipo utakapoweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unawezaje kumwambia ndugu yako: Ngoja, ndugu yangu, nikitoe kibanzi kilichomo jichoni mwako? Nalo gogo lililomo jichoni mwako mwenyewe hulioni? Mjanja, kwanza litoe gogo katika jicho lako! Kisha utazame vema, ndivyo upate kukitoa kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Au, namna gani unaweza kumwambia ndugu yako kwamba aache umwondoe vumbi inayokuwa ndani ya jicho lake, wakati ndani ya jicho lako mungali ile nguzo. Wewe munafiki, ondosha kwanza nguzo kutoka ndani ya jicho lako, kisha utaweza kuona waziwazi na kuweza kuondosha ile vumbi inayokuwa ndani ya jicho la ndugu yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Au wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, niache niondoe kibanzi kilichomo jichoni mwako, na wewe mwenyewe huioni boriti iliyomo jichoni mwako? Mnafiki, toa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako, ndipo utakapoona vema kutoa kibanzi jichoni mwa ndugu yako.