Luke 6:44 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila mti unatambuliwa kutokana na aina ya matunda unayozaa. Huwezi kupata tini kwenye vichaka vya miiba. Na huwezi kuchuma zabibu kwenye michongoma!
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba wala zabibu kwenye michongoma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani kila mti hutambulikana kwa matunda yake mwenyewe. Kwani hawachumi kuyu miibani, wala hawachumi zabibu katika mikunju.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kila muti unajulikana kwa njia ya matunda yake. Watu hawachumi matunda ya tini au mizabibu juu ya miti ya miiba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana killa mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa kuwa katika miiba hawachumi tini, wala katika michongoma hawachumi zabibu.