Luke 6:48 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ni kama mtu anayejenga nyumba, huchimba chini sana, na kujenga nyumba yake kwenye mwamba. Mafuriko yanapokuja, huigonga nyumba kwa nguvu, nyumba hiyo haiwezi kuanguka kwa kuwa imejengwa vizuri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye ni kama mtu anayejenga nyumba, akachimba chini sana na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, maji ya ghafula yakaipiga ile nyumba lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri juu ya mwamba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, maji ya ghafula yaliipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliipiga nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Amefanana na mtu aliyejenga nyumba, akiichimbia chini vizuri na kuweka msingi mwambani. Maji yalipojaa yakatoka mto, ukapasua penye ile nyumba, lakini haukuweza kuitingisha, kwa kuwa ilikuwa imejengwa vizuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
anafananishwa na mutu aliyejenga nyumba, akaichimbia musingi chini sana mpaka kwenye jiwe, na kuujenga pale. Mvua kubwa iliponyesha, muto ukajaa na maji yakashambulia nyumba ile, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba.