Luke 6:49 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini watu wanaoyasikia maneno yangu na hawayatii ni kama mtu anayejenga nyumba bila kutayarisha msingi. Mafuriko yanapokuja, nyumba huanguka chini kwa urahisi na kubomoka kabisa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini yeyote anayesikia maneno yangu lakini asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yeye ayasikiaye maneno yangu na asiyatende ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya mchanga bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaipiga kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini anayeyasikia asipoyafanyiza amefanana na mtu aliyejenga nyumba mchangani pasipo msingi. Basi, mto ulipotokea na kupasua hapo, ilianguka papo hapo, kupasuka kwake ile nyumba kukawa kukubwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini yule anayesikia maneno yangu pasipo kuyashika, anafananishwa na mutu aliyejenga nyumba juu ya udongo bila kuchimba musingi. Maji kutoka muto yakaishambulia, na mara moja ikaanguka na kubomoka kabisa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae asikiae bila kutenda afanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo pasipo msingi: bassi mto ukairukia kwa nguvu, ikaanguka marra, na kuanguka kwake ile nyumba kulikuwa kukubwa.