Luke 6:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waalimu wa sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisa cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walimu wa sheria na Mafarisayo walikuwa wakimvizia Yesu. Walikuwa wanasubiri waone ikiwa ataponya siku hiyo ya Sabato. Walitaka kumwona akifanya jambo lolote lililo kinyume ili wamshitaki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walimu wa Sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisingizio cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waalimu wa sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisa cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu, hivyo wakawa wanamwangalia kwa karibu ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kama ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waalimu wa sheria na Mafarisayo walitaka kupata kisa cha kumshtaki Yesu na hivyo wakawa wanangojea waone kama angemponya mtu siku ya Sabato.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waandishi na Mafariseo wakamtunduia, kama atamponya siku ya mapumziko, waone neno la kumsuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kwamba ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walimu wa Sheria na Wafarisayo wakamuchunguza Yesu kusudi waone kama ataponyesha mutu kwa siku ya Sabato. Walifanya vile kusudi wapate sababu ya kumushitaki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mafarisavo na waandishi wakamvizia kuona kwamba ataponya siku ya Sabato, wapate kumshitaki.