Luke 6:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa Torati na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Yesu akawaambia, “Ninawauliza ninyi, Sheria inaturuhusu tufanye nini siku ya Sabato: kutenda mema au kutenda mabaya? Je, ni halali kuokoa uhai au kuuangamiza?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yesu akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, akisema, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato, kutenda mema au kutenda mabaya? Kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa Torati na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu akawaambia, “Nawaulizeni, je, ni halali siku ya Sabato kutenda jambo jema au kutenda jambo baya; kuokoa maisha au kuyaangamiza?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yesu akawaambia: Nawauliza ninyi: Iko ruhusa siku ya mapumziko kufanya mema au kufanya maovu? kuponya roho ya mtu au kuiangamiza?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akawaambia: “Ninawauliza: Sheria inaturuhusu kufanya mema au mabaya kwa siku ya Sabato? Kuponyesha mutu au kumwua?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia, Nitawaulizeni neno moja. Ni halali siku ya Sabato kutenda mema au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua?