Luke 7:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote kwa watu waliokuwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipomaliza kuwaambia watu mambo yote aliyotaka kuwaambia, alikwenda mjini Kapernaumu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya Yesu kumaliza kusema haya yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kusema yale aliyotaka watu wasikie, Yesu alikwenda Kafarnaumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipokwisha kuyasema maneno yake yote, watu wakimsikiliza, akaenda, akaingia Kapernaumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu, aliingia Kapernaumu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokwisha kusema maneno hayo yote kwa watu waliomusikiliza, akaenda Kapernaumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ALIPOKWISHA kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu akaingia Kapernaum.