Luke 7:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baadaye kidogo, Isa alienda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walienda pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata Yesu na wafuasi wake walikwenda katika mji wa Naini. Kundi kubwa la watu walisafiri pamoja nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baadaye kidogo Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake pamoja na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walikwenda pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baadaye kidogo, Isa alikwenda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walikwenda pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadaye kidogo alikwenda mpaka katika mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja uitwao Naini, na wafuasi wake na kundi kubwa la watu waliandamana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Kisha punde kidogo akashika njia kwenda katika mji, jina lake Naini. Wakafuatana naye wanafunzi wake na kundi la watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kesho yake nyuma ya maneno haya, Yesu akaenda katika muji Naina, nao wanafunzi wake na kundi kubwa la watu wakamufuata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa khalafu yake, akaenda mji uitwao Nain, wanafunzi wake na watu wengi wakafuatana nae.