Luke 7:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mwanamke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alipolikaribia lango la mji, aliona watu wamebeba maiti. Alikuwa ni mwana pekee wa mama mjane. Watu wengi kutoka mjini walifuatana na yule mama mjane.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya kijana mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wengi mjini walikuwa pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipolikaribia lango la mji, panatolewa mfu; huyu alikuwa mwana wa pekee wa mama yake, naye alikuwa mjane. Kwa hiyo watu wengi wa mji ule walikwenda pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipokaribia kwenye mulango wa ukuta wa muji, kukatokea watu wanaobeba maiti ya kijana mumoja aliyekuwa mutoto wa pekee wa mama mumoja mujane. Nao watu wengi wa muji ule walikuwa wakimusindikiza yule mama.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae.