Luke 7:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, akaenda akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wamelichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akalikaribia jeneza, akaligusa. Nao wale waliokuwa wamelibeba wakasimama. Akasema, “Kijana, nakuambia, inuka.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akakaribia, akaligusa jeneza. Wanaume waliokuwa wamebeba jeneza wakasimama. Ndipo Yesu akamwambia kijana aliyekufa, “Kijana, nakuambia, inuka!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akaenda, akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wanalichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, akaenda akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wamelichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akasogea mbele akaligusa lile jeneza na wale waliokuwa wamelibeba wakasimama kimya. Akasema, “Kijana, nakuambia inuka.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akasogea mbele akaligusa lile jeneza na wale waliokuwa wamelibeba wakasimama kimya. Akasema, “Kijana, nakuambia inuka.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, akaenda akaligusa lile jeneza, na wale waliokuwa wamelichukua wakasimama. Halafu akasema, “Kijana! Nakuamuru, amka!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika karibu, alishike jeneza, wachukuzi wakasimama. Akasema: Kijana, nakuambia: Inuka!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akajongea, akagusa sanduku, nao watu waliokuwa wakilibeba wakasimama. Akasema: “Kijana, ninakuamuru, amuka!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka.