Luke 7:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Afisa wa jeshi katika mji wa Kapernaumu alikuwa na mtumishi aliyekuwa wa muhimu sana kwake. Mtumishi huyu alikuwa mgonjwa sana karibu ya kufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huko kulikuwa na jemadari mmoja Mroma ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu kufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu ya kufa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu kufa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtumwa wake afisa mmoja alikuwa mgonjwa, karibu kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukawako mkubwa wa askari mwenye mtumwa, ambaye alipendezwa sana naye; huyu alikuwa mgonjwa wa kufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kule kulikuwa mukubwa mumoja wa waaskari aliyekuwa na mutumishi wake mupendwa sana. Mutumishi yule alikuwa mugonjwa karibu kufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana.