Luke 7:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: ‘Wewe ndiye yule anayekuja, au tumngoje mwingine?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu walipofika kwa Isa wakamwambia, “Yahya ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiwe yule aliyekuwa aje, au tumtazamie mwingine?’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wa Yohana walipofika kwa Yesu, wakasema, “Yohana Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: ‘Wewe ndiye yule ajaye, au tumsubiri mwingine?’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: Wewe ndiye yule ajaye, au tumtazamie mwingine?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: ‘Wewe ndiye yule anayekuja, au tumngoje mwingine?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu walipofika kwa Yesu wakamwambia, “Yohana Mbatizaji ametutuma tukuulize, ‘Je, wewe ndiye yule ajaye au tumtazamie mwingine?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu walipofika kwa Isa wakamwambia, “Yahya ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanafunzi walipomfikia Yesu wakamwambia, “Yohane Mbatizaji ametutuma kwako tukuulize: ‘Wewe ndiye yule anayekuja, au tumngoje mwingine?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Waume hao walipofika kwake wakasema: Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, tuulize: Wewe ndiwe mwenye kuja, au tungoje mwingine?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wanafunzi walipofika kwa Yesu wakamwambia: “Yoane Mubatizaji ametutuma kwako kukuuliza ikiwa wewe ndiwe yule aliyepaswa kuja au tumungojee mwingine.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi watu hawo walipofika kwake wakasema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiye ajae au tumtazamie mwingine?