Luke 7:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: Vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yahya yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha aliwaambia wanafunzi wa Yohana, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mliyoyaona na kuyasikia: wasiyeona wanaona, walemavu wa miguu wanatembea, wenye magonjwa mabaya ya ngozi wanatakasika, wasiyesikia wanasikia. Waliokufa wanafufuliwa na Habari Njema inahubiriwa kwa maskini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari njema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yohana yote mliyoyaona na kuyasikia. Vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wahubiriwa Habari Njema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yahya yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yesu akawajibu, “Nendeni mkamwambie Yohane yale mliyojionea na kuyasikia: Vipofu wanaona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu akiwaambia: Rudini, mmsimulie Yohana, mliyoyaona nayo mliyoyasikia: vipofu wanaona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanapigiwa mbiu njema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Yesu akawajibu wale wajumbe: “Mwende kumwelezea Yoane mambo muliyoona na kusikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanapata kusikia, wafu wanafufuliwa na Habari Njema inahubiriwa kwa wamasikini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema: