Luke 7:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, “Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya wanafunzi wa Yohana kuondoka, Yesu akaanza kuwaambia watu kuhusu Yohana, “Mlitoka kwenda jangwani kuona nini? Mtu aliyekuwa dhaifu, kama unyasi unaotikiswa na upepo?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kule jangwani, hivi mlitaka kuona kitu gani? Mlitaka kuona unyasi unaotikiswa na upepo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuuambia ule umati wa watu kuhusu Yohana: “Mlipokwenda nyikani mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na makutano kuhusu Yahya. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo wajumbe wa Yohane walipokwisha kwenda zao, Yesu alianza kuyaambia makundi ya watu juu ya Yohane: “Mlikwenda kutazama nini kule jangwani? Je, mlitaka kuona mwanzi unaotikiswa na upepo?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wajumbe wa Yohana walipokwisha kwenda zao, akaanza kusema na yale makundi ya watu mambo ya Yohana: Mlipotoka kwenda nyikani mlikwenda kutazama nini? Mlikwenda kutazama utete unaotikiswa na upepo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wajumbe wa Yohana walipokwisha ondoka, alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale wajumbe wa Yoane walipokwisha kuondoka, Yesu akaanza kuwaambia makundi ya watu habari za Yoane akisema: “Mulienda katika jangwa kuangalia nini? Tete linalotikiswa na upepo? Hapana!
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale wajumbe wa Yohana, walipokwisha kwenda zao, akaanza kuwaambia makutano khabari za Yohana, Mlitoka kwenda jangwani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?