Luke 7:25 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevaa mavazi maridadi? Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mlitegemea kuona nini? Mtu aliyevaa mavazi mazuri? Hakika si hilo. Watu wanaovaa mavazi mazuri na kuishi kwa anasa wako katika majumba ya wafalme.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevalia mavazi maridadi? La hasha! Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevaa mavazi maridadi? Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya fahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya fahari na kuishi maisha ya anasa hukaa katika majumba ya kifalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokaa kwa raha, wamo katika majumba ya kifalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona mtu aliyevaa mavazi maridadi? Wanaovaa mavazi maridadi na kuishi maisha ya anasa, hukaa katika majumba ya wafalme!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Au mlitoka kutazama nini? Mlikwenda kutazama mtu aliyevaa mavazi mororo? Tazameni, wanaovaa mavazi yenye utukufu na kula vya mali wamo nyumbani mwa wafalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Jueni, watu wenye mavazi ya utukufu, wanaokula raha, wamo katika majumba ya kifalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi mulienda kuangalia nini? Mutu aliyevaa nguo nzuri? Hapana! Wale wanaovaa nguo za bei kali na kuishi katika raha wanakaa katika nyumba za kifalme.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi meroro? Fahamuni, watu wenye nguo za umalidadi na kuishi maisha ya anasa wamo katika majumba ya wafalme.