Luke 7:29 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliposikia hayo watu wote na watozaushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Watu wote, hata watoza ushuru, waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
(Watu waliposikia hili, wote walikubali kuwa mafundisho ya Mungu yalikuwa mazuri. Hata watoza ushuru waliobatizwa na Yohana walikiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Waliposikia hayo watu wote na watoza ushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliposikia hayo watu wote na watozaushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Yesu, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni mwema, maana walikuwa wamebatizwa na Yohana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliposikia hayo watu wote na watozaushuru waliusifu wema wa Mungu; hao ndio wale waliokuwa wameupokea ubatizo wa Yohane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wote waliomsikia, hata watoza kodi wakauitikia wongofu wake Mungu, wakabatizwa ubatizo wa Yohana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wote na watoza ushuru waliposikia hayo, waliikiri haki ya Mungu, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
(Watu wote waliomusikiliza, na walipishaji wa kodi vilevile, wakakubali kwamba Mungu ni mwenye haki, hata wakabatizwa na Yoane.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.