Luke 7:36 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani kwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Farisayo mmoja alimwalika Isa kwake ale chakula. Hivyo Isa akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kuketi mezani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mmoja wa Mafarisayo alimwalika Yesu kula chakula nyumbani mwake. Yesu akaenda nyumbani kwa yule Farisayo, akaketi katika nafasi yake sehemu ya kulia chakula.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani mwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani kwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chakula. Hivyo Yesu akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kukaa katika nafasi yake mezani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Farisayo mmoja alimwalika Isa nyumbani kwake kwa chakula. Hivyo Isa akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kukaa katika nafasi yake mezani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfarisayo mmoja alimwalika Yesu kula chakula nyumbani kwake. Akaingia nyumbani kwa huyo Mfarisayo, akakaa kula chakula.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Fariseo mmoja alipomwalika, ale pamoja naye, akaingia nyumbani mwa yule Fariseo, akakaa chakulani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Mufarisayo mumoja akamwalika Yesu kwake kuja kula chakula. Basi Yesu akaenda kwenye nyumba ya yule Mufarisayo, na kuikaa kula chakula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu mmoja katika Mafarisayo akamtaka ale chakula pamoja nae. Akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.