Luke 7:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Palikuwa na mwanamke mmoja katika mji ule aliyekuwa mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Isa alikuwa akila chakula nyumbani mwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alikuwepo mwanamke mmoja katika mjini ule aliyekuwa na dhambi nyingi. Alipojua kuwa Yesu alikuwa anakula chakula nyumbani kwa Farisayo, alichukua chupa kubwa yenye manukato ya thamani sana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja aliyekuwa anaishi maisha mabaya. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye mwanamke mmoja kwenye ule mji, ambaye alikuwa mwenye dhambi, alipojua kwamba Yesu alikuwa akila chakula nyumbani kwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marmar yenye manukato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye mwanamke mmoja kwenye ule mji, ambaye alikuwa mwenye dhambi, alipojua kwamba Isa alikuwa akila chakula nyumbani kwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, katika mji ule kulikuwa na mama mmoja mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Yesu yuko nyumbani kwa huyo Mfarisayo, alichukua chupa ya alabasta yenye marashi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mjini mle mlikuwa na mwanamke mkosaji. Naye alipotambua, ya kuwa yumo mwa yule Fariseo, amekaa chakulani, akaja na kichupa cha manukato,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, mwanamke mmoja wa mji ule, aliyekuwa mwenye dhambi, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika muji ule kulikuwa mwanamuke mumoja aliyejulikana kuwa mwenye mwenendo mubaya. Mwanamuke yule alipopata habari kama Yesu alikuwa akikula ndani ya nyumba ya yule Mufarisayo, akafika akileta chupa la jiwe linalojaa marasi ya bei kali.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kumbe! Mwanamke mmoja katika mji ule ahyekuwa mwenye dhambi, alipopata khabari ya kuwa ameketi katika nyumba ya yule Farisayo, akaleta chupa cha alabastro yenye marhamu,