Luke 7:38 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Isa akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alisimama karibu na miguu ya Yesu akilia. Kisha alianza kuisafisha miguu ya Yesu kwa machozi yake na akaifuta kwa nywele zake, akaibusu mara nyingi na kuipaka manukato.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke akiwa amesimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake akaibusu na kuimiminia manukato.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Isa akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusubusu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaja, akasimama karibu na miguu yake Yesu, akilia, na machozi yake yakamdondokea Yesu miguuni. Huyo mwanamke akaipangusa miguu ya Yesu kwa nywele zake. Kisha akaibusu na kuipaka yale marashi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akamsimamia nyuma miguuni pake mwenye machozi, akaanza kuyadondosha miguuni pake, akayasugua kwa nywele za kichwani pake, akainonea miguu yake, kisha akaipaka manukato.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akakuja kuinama kwenye miguu ya Yesu, akilia. Machozi yake yakamwangika juu ya miguu ya Yesu, akaipanguza na nywele zake, akaibusu na kuipakaa marasi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumchuruzia miguu kwa machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake akibusu sana miguu yake, na kuipaka yale marhamu.