Luke 7:39 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule Farisayo aliyemwalika Isa alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona hili, alijisemea moyoni mwake, “Mtu huyu angekuwa nabii, angetambua kuwa mwanamke huyu anayemgusa ni mwenye dhambi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule Farisayo aliyemwalika Isa alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule Mfarisayo aliyemwalika Yesu alipoona hayo, akawaza moyoni mwake, “Kama mtu huyu angekuwa kweli nabii angejua huyu mwanamke ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule Fariseo aliyemwalika alipoviona akasema moyoni mwake: Huyu kama angekuwa mfumbuaji, angemtambua mwanamke huyu anayemgusa, kama ni nani, kama ni wa namna gani, kwamba ni mkosaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule Mufarisayo aliyemwalika Yesu alipoona vile, akajisemesha: “Kama mutu huyu angekuwa kweli nabii, angetambua mwanamuke huyu anayemugusa ni wa namna gani. Angetambua kwamba yeye ni mwenye mwenendo mubaya.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.