Luke 7:41 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: Mmoja alikuwa amekopa denari 500, na mwingine hamsini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari mia tano na mwingine dinari hamsini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akasema, “Kulikuwa watu wawili. Wote wawili walikuwa wanadaiwa na mkopeshaji mmoja. Mmoja alidaiwa sarafu mia tano za fedha, na wa pili sarafu hamsini za fedha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa dinari mia tano, na mwingine hamsini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: mmoja alikuwa amekopa denari 500, na mwingine hamsini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari 500 na mwingine dinari hamsini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari 500 na mwingine dinari hamsini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu wawili walikuwa wamemkopa mtu fedha: Mmoja alikuwa amekopa denari 500, na mwingine hamsini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili. Wa kwanza deni lake ni shilingi 500, mwenzake 50.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akasema: “Kulikuwa watu wawili waliokopesha feza kutoka kwa mutu mumoja. Mumoja alikuwa na deni ya vikoroti mia tano vya feza na mwingine vikoroti makumi tano.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili: mmoja aliwiwa nae dinari khamsi mia, na wa pili khamsini.