Luke 7:47 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo nakuambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninakwambia kuwa dhambi zake zilizo nyingi zimesamehewa. Hii ni wazi, kwa sababu ameonesha upendo mkubwa. Watu wanaosamehewa kidogo hupenda kidogo.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo nakuambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo nakuambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehewa kidogo, hupenda kidogo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nakuambia: Ameondolewa makosa yake yaliyo mengi, kwani mapendo yake ni mengi. Lakini anayeondolewa machache tu, naye mapendo yake ni machache.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hayo nakuambia, Amesamehewa dhambi zake ambazo ni nyingi, kwa kuwa amependa sana; lakini asamehewaye kidogo, huyo hupenda kidogo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa sababu hii ninakuambia kwamba upendo ambao mwanamuke huyu alioonyesha unahakikisha kwamba Mungu amemusamehe zambi zake zinazokuwa nyingi. Lakini yule anayesamehewa kwa machache haonyeshi upendo zaidi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo.