Luke 8:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo, Yesu alipitia mijini na vijijini akitangaza Habari Njema za ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya haya Isa alienda, akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri Injili ya ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku iliyofuata, Yesu alisafiri kupitia katika baadhi ya miji na vijiji. Yesu aliwahubiri watu Habari Njema kuhusu ufalme wa Mungu. Mitume kumi na wawili walikuwa pamoja naye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya hayo, Yesu alipitia katika miji na vijiji akitangaza Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo, Yesu alipitia mijini na vijijini akitangaza Habari Njema za ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya haya Yesu alikwenda akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya haya Isa alikwenda, akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza Habari Njema ya ufalme wa Mungu; na wale Kumi na Wawili walikuwa pamoja naye,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo, Yesu alipitia mijini na vijijini akitangaza Habari Njema za ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akatembea na kuingia mwenyewe mji kwa mji na kijiji kwa kijiji, akiutangaza Utume mwema wa ufalme wa Mungu nao wale kumi na wawili walikuwa pamoja naye,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya pale Yesu akapita katika miji na vijiji mbalimbali, akihubiri na kutangaza Habari Njema ya Ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walienda naye
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae,