Luke 8:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akasema, “Ninyi mmepewa ujuzi wa siri za ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanatazama, wasione; ingawa wanasikiliza, wasielewe.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akasema, “Mmechaguliwa kujua kweli za siri kuhusu ufalme wa Mungu. Lakini ninatumia mafumbo kuzungungumza na watu wengine. Ninafanya hivi ili, ‘Watazame, lakini wasiweze kuona. Wasikia, lakini wasielewe.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akajibu, “Ninyi mmejaliwa kujua siri za Ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akasema, “Ninyi mmejaliwa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanaona, wasione; ingawa wanasikia, wasielewe.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akasema, “Ninyi mmepewa kufahamu siri za Ufalme wa Mwenyezi Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanatazama, wasione; ingawa wanasikiliza, wasielewe.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akasema: Ninyi mmepewa kuyatambua mafumbo ya ufalme wa Mungu, lakini wale wengine huambiwa kwa mifano, kusudi watazame, lakini wasione, wasikilize, lakini wasijue maana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawajibu: “Ninyi mumefunuliwa kujua siri ya Ufalme wa Mungu, lakini kwa watu wengine si vile. Wao wanaambiwa maneno hayo kwa njia ya mifano, kusudi waangalie, lakini wasione kitu, nao wasikie, lakini wasifahamu kitu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.