Luke 8:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zile zilizoanguka njiani zinaonesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini wakaokoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zile zilizoanguka kando ya njia ni wale ambao husikia neno, naye ibilisi anakuja na kuliondoa neno kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengine ni kama mbegu zilizoanguka njiani. Husikia mafundisho ya Mungu, lakini Shetani huja na kuwafanya waache kuyatafakari. Hii huwafanya kutoamini na kuokoka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zile zilizoanguka njiani zinaonyesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini na hivyo wakaokoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zile zilizoanguka njiani zinaonesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini wakaokoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zile zilizoanguka kando ya njia, ni wale ambao husikia neno na ibilisi huja na kuliondoa kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zile zilizoanguka kando ya njia ni wale ambao husikia neno, naye ibilisi anakuja na kuliondoa neno kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zile zilizoanguka njiani zinaonesha watu wale wanaosikia lile neno, halafu Ibilisi akaja na kuliondoa mioyoni mwao wasije wakaamini wakaokoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zilizoko njiani ndio wenye kulisikia; kisha huja Msengenyaji, akaliondoa Neno mioyoni mwao, wasipate kulitegemea na kuokoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na kuokoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nafasi ile mbegu zilipoanguka pembeni ya njia ni mufano wa watu wanaosikia neno la Mungu. Lakini Shetani anakuja na kuondoa lile neno katika mioyo yao kusudi wasiamini na kuokolewa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale wa njiani, ndio wasikiao, ndipo huja Shetani na kulitoa lile neno mioyoni mwao, illi wasije wakaamini, wakaokoka.