Luke 8:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zile zilizoanguka penye mawe zinaonesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Lakini kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zile mbegu zilizoanguka kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa muda mfupi, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wengine wanafanana na mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye mawe. Ni watu ambao huyasikia mafundisho ya Mungu na kuyapokea kwa furaha, lakini kwa kuwa hawana mizizi yenye kina, huamini kwa muda mfupi. Majaribu yanapokuja, humwacha Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zile zilizoanguka penye mawe zinaonyesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Hata hivyo, kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zile zilizoanguka penye mawe zinaonesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Lakini kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zile za kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa kitambo kidogo, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zile mbegu zilizoanguka kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa muda mfupi, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zile zilizoanguka penye mawe zinaonesha watu wale ambao wanaposikia juu ya lile neno hulipokea kwa furaha. Lakini kama zile mbegu, watu hao hawana mizizi maana husadiki kwa kitambo tu, na wanapojaribiwa hukata tamaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo zilizoko mwambani ndio hao: wanapolisikia Neno hulipokea kwa furaha, lakini hawana mizizi, hulitegemea kitambo kidogo, kisha siku za kujaribiwa hujitenga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale penye mwamba ndio wale ambao wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Udongo wenye mawe pahali mbegu zilipoanguka ni mufano wa watu wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha, lakini halizami ndani yao kama mizizi. Wanaliaminia kwa muda mufupi tu, nayo majaribu yanapowafikia, wanaliacha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.