Luke 8:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho, kitachukuliwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, kuweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana yeyote aliye na kitu atapewa zaidi. Lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho atanyang’anywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo yatafakarini kwa umakini yale mnayosikia. Watu wenye uelewa kiasi watapokea zaidi. Lakini wale wasio na uelewa watapoteza hata ule wanaodhani kuwa wanao.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani kuwa anacho, kitachukuliwa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho, kitachukuliwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, iweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana ye yote aliye na kitu atazidishiwa na ye yote asiye nacho, hata kile anachodhani anacho atanyang'anywa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, kuweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana yeyote aliye na kitu atapewa zaidi. Lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho atanyang’anywa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kwa hiyo, jihadharini jinsi mnavyosikia; maana aliye na kitu ataongezewa, lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho, kitachukuliwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, mwangalie, jinsi mnavyosikia! Kwani aliye na mali atapewa; lakini asiye na kitu atachukuliwa hata kile, alichokiwaza kuwa chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang’anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Basi mufanye angalisho na jinsi munavyosikia maneno. Kwa maana mutu anayekuwa na kitu, ataongezewa kingine, lakini mutu asiyekuwa na kitu, atanyanganywa kile anachozania kuwa nacho.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jihadharini, bassi, jinsi msikiavyo. Maana yeye aliye na kitu, atapewa: nae asiye na kitu ataondolewa hatta kitu kile ambacho anaonekana kuwa anacho.