Luke 8:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Siku moja Yesu na wafuasi wake walipanda mashua. Akawaambia, “Tuvuke mpaka upande mwingine wa ziwa.” Wakaanza safari kuvuka ziwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ng'ambo.” Basi, wakaanza safari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ng'ambo.” Basi, wakaanza safari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja Yesu alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Twendeni tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ng’ambo ya ziwa.” Nao wakaondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa siku zile mojawapo alipanda katika mashua yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja, Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvuke ziwa twende mpaka ngambo.” Basi, wakaanza safari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa siku moja, mwenyewe akajipakia chomboni na wanafunzi wake, akawaambia: Tuvuke kwenda ng'ambo ya ziwa! Wakatweka matanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Yesu akaingia ndani ya chombo pamoja na wanafunzi wake. Naye akawaambia: “Tuvuke ngambo ya ziwa.” Basi wakaondoka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.