Luke 8:23 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walipokuwa wanasafiri, Yesu alisinzia. Tufani kubwa ikalikumba ziwa na mashua ikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, mashua ikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipokuwa wanasafiri kwa mashua, Yesu alishikwa na usingizi, akalala. Dhoruba kali ikaanza kuvuma, maji yakaanza kuingia ndani ya mashua, wakawa katika hatari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipoendelea baharini, akalala usingizi. Kukashuka msukosuko wa upepo ziwani, chombo kikajaa maji, wakafikisha kuangamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao walipokuwa wakivuka ziwa, Yesu akalala usingizi. Mara moja zoruba kali ikaanza kuvuma, hata maji yakaanza kuingia ndani ya chombo, nao wakakuwa katika hatari.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipokuwa wakienda kwa matanga akalala usingizi. Ikashuka dharuba ya upepo juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika khatari.