Luke 8:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana! Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaukemea upepo na mawimbi ya maji, navyo vikatulia, kukawa shwari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, Bwana, tunaangamia!” Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wakamwendea, wakamwamsha, wakasema, “Mkuu, mkuu, tutazama!” Yesu akasimama, akaukemea upepo na mawimbi ya maji. Upepo ukakoma na ziwa likatulia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana! Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaikemea dhoruba na mawimbi, navyo vikatulia, kukawa shwari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana! Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaukemea upepo na mawimbi ya maji, navyo vikatulia, kukawa shwari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakipiga kelele, wakisema, “Bwana, Bwana, tunaangamia!” Yeye akaamka akaukemea ule upepo na yale mawimbi, vikakoma, pakawa shwari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, Bwana, tunaangamia!” Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wale wanafunzi wakamwendea Yesu, wakamwamsha wakisema, “Bwana, Bwana! Tunaangamia!” Yesu akaamka, akaukemea upepo na mawimbi ya maji, navyo vikatulia, kukawa shwari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipomjia, wakamwamsha wakisema: Bwana, Bwana, tunaangamia! Naye alipoinuka, akaukaripia upepo na mawimbi ya maji, yakatulia, kukawa kimya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wanafunzi wake wakamujongelea, wakamwamusha wakisema: “Bwana, Bwana, tunakufa!” Yesu alipoamuka, akakaripia zoruba, nayo ikakoma na maji yakatulia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Mwalimu, Mwalimu, tunaangamia. Akaondoka, akaukemea upepo, na msukosuko wa maji, vikakoma, kukawa shwari.