Luke 8:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawaambia, “Iko wapi imani yenu?” Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Yesu akawaambia wafuasi wake, “Imani yenu iko wapi?” Lakini wao waliogopa na kustaajabu, wakanong'onezana, “Huyu ni mtu wa namna gani? Anaamuru upepo na maji, na vinamtii?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akawaambia, “Iko wapi imani yenu?” Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawaambia, “Iko wapi imani yenu?” Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni mtu wa namna gani ambaye anaamuru hata upepo na maji navyo vikamtii?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawaambia, “Iko wapi imani yenu?” Lakini wao walishangaa na kuogopa huku wakiambiana, “Huyu ni nani basi, hata anaamuru dhoruba na mawimbi, navyo vinamtii?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawaambia: Tegemeo lenu liko wapi? Kwa kuogopa wakastaajabu tu, wakasemezana wao kwa wao: Ni mtu gani huyu, ya kuwa anaagiza hata upepo na maji, nayo yanamtii!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akawaambia wanafunzi wake: “Imani yenu iko wapi?” Nao wakaogopa na kushangaa, wakiulizana: “Huyu ni mutu gani? Anaamuru hata zoruba na ziwa, navyo vinamutii!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakastaajabu, wakasemezana, Huyu ni nani, bassi, kwa kuwa hatta upepo na bahari aviamuru vikamtii?