Luke 8:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipomwona Yesu, alijitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kubwa, “We, Yesu Mwana wa Mungu Mkuu, una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomwona Isa, alipaza sauti, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pepo aliyekuwa ndani yake alikuwa akimpagaa mara nyingi na alikuwa akifungwa gerezani, mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa minyororo. Lakini kila mara aliivunja. Pepo ndani yake alikuwa anamlazimisha kwenda nje ya mji mahali pasipoishi watu. Yesu alimwamuru kumtoka mtu yule. Alipomwona Yesu, alianguka mbele yake huku akipiga kelele kwa sauti, “Unataka nini kwangu, Yesu, Mwana wa Mungu Mkuu Aliye Juu? Tafadhali usiniadhibu!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipomwona Yesu, alipiga kelele na kujitupa chini mbele yake, na kusema kwa sauti kubwa “We, Yesu Mwana wa Mungu Aliye Juu una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipomwona Yesu, alijitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kubwa, “We, Yesu Mwana wa Mungu Mkuu, una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomwona Yesu alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, “Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomwona Isa, alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu? Nakusihi usinitese.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipomwona Yesu, alijitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kubwa, “We, Yesu Mwana wa Mungu Mkuu, una shauri gani nami? Ninakusihi usinitese!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomwona Yesu akapiga kelele, akamwangukia, akapaza sauti akisema: Tuko na jambo gani, mimi na wewe Yesu, Mwana wa Mungu Alioko huko juu? Nakuomba wewe, usiniumize.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati alipomwona Yesu, akalalamika na kuanguka mbele yake, na kusema kwa nguvu: “Yesu, Mwana wa Mungu Mukubwa, kuna neno kati yako na mimi? Ninakusihi, usinitese!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipomwona Yesu, akapiga kelele, akamwangukia, akasema kwa sauti kuu. Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuomba usiniadhibu.