Luke 8:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” — kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Mtu yule akajibu, “Jeshi.” (Alisema jina lake ni “Jeshi” kwa sababu pepo wengi walikuwa wamemwingia.)
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni Jeshi” —kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” — kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Yeye akajibu, “Jina langu ni ‘Jeshi’” – kwa sababu pepo wengi walikuwa wamempagaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipomwuliza: Jina lako nani? akasema: Maelfu. Kwani alikuwa ameingiwa na pepo wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamwuliza: “Jina lako nani?” Naye akamujibu: “Jina langu ni ‘Jeshi.’ ” Alisema vile kwa sababu ndani ya mutu yule mulikuwa pepo wengi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akamwuliza, akisema, Jina lako nani? Akasema, Legioni, kwa sababu pepo wengi wamemwingia.