Luke 8:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali hapo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Katika kilima kile, kulikuwa kundi kubwa la nguruwe wakichungwa. Pepo wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie wale nguruwe. Hivyo Yesu akawaruhusu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali hapo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo karibu wakilisha kandokando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilishwa mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali hapo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha mlimani. Basi, hao pepo wakamsihi awaruhusu wawaingie. Naye Yesu akawapa ruhusa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, kulikuwako kundi la nguruwe wengiwengi waliokuwako malishoni mlimani. Wakambembeleza, awape ruhusa ya kuwaingia wale. Alipowapa ruhusa,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, hapo palikuwa na kundi la nguruwe wengi wakilisha mlimani; wakamsihi awape ruhusa kuwaingia wale. Akawapa ruhusa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na karibu na pale kulikuwa kundi la nguruwe wengi waliokuwa wakijitafutia chakula kwenye mulima. Wale pepo wakamusihi Yesu awaruhusu kuingia ndani ya wale nguruwe. Naye akawaruhusu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kulikuwako kundi la nguruwe wengi, wakilisha mlimani. Wakamsihi awape rukhusa kuwaingia wao.