Luke 8:42 — Compare Translations
13 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na mbili, alikuwa anakufa. Isa alipokuwa akienda, umati wa watu wakamsonga sana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwana wa pekee mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa mahututi. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Isa alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa binti yake yu karibu kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, watu wakawa wanamsonga kila upande.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani mwanawe wa kike wa pekee aliyekuwa mwenye miaka 12 aliingia kufani. Alipokwenda naye, watu wengi sana wakamsongasonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa binti yake yu katika kufa, ambaye ni mwana pekee, umri wake amepata miaka kumi na miwili. Na alipokuwa akienda makutano walimsonga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu alikuwa na mutoto mumoja binti wa pekee mwenye umri wa miaka yapata kumi na miwili, na aliyekuwa karibu kufa. Yesu alipokuwa akienda kule, kundi kubwa la watu walimusongasonga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga.