Luke 8:43 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili; ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, [na alikuwa amegharimia mali yake yote kwa matibabu] lakini hakuna yeyote aliyeweza kumponya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke aliyekuwa akitokwa damu kwa miaka kumi na mbili alikuwepo katika umati huo. Alikuwa ametumia mali zake zote kwa madaktari, lakini hakuna daktari aliyeweza kumponya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili; ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika umati huo alikuwepo mwanamke mmoja aliyekuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna ye yote aliyeweza kumponya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika umati huo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna yeyote aliyeweza kumponya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu yeyote,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kulikuwa na mwanamke mmoja kati ya lile kundi la watu, ambaye alikuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili; ingawa alikuwa amekwisha tumia mali yake yote kwa waganga, hakuna aliyefaulu kumponya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kukawa na mwanamke mwenye ugonjwa wa kutoka damu tangu miaka 12. Kwa kuwa hakuweza kuponywa na mtu ye yote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kati yao kulikuwa mwanamuke mumoja mwenye ugonjwa wa kutokwa na damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Alikuwa ametumia mali yake yote kwa kulipa waganga, lakini hakuna hata mumoja wao ambaye aliweza kumuponyesha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu tangu miaka thenashara, aliyegharimu vitu vyote alivyo navyo akawapa tabibu asipate kuponywa na mtu aliye yote,