Luke 8:47 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yule mwanamke alipoona ya kwamba hataweza kujificha akajitokeza akitetemeka. Akasujudu mbele ya Yesu. Huku kila mmoja akisikia, akaeleza sababu iliyomfanya amguse, na kwamba alipona wakati ule ule alipomgusa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponyeshwa mara moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Yesu, akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mwanamke alipoona kwamba hawezi kujificha, akajitokeza akitetemeka kwa hofu, akajitupa mbele ya Yesu. Hapo akaeleza mbele ya wote kisa cha kumgusa Yesu na jinsi alivyoponywa mara moja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mwanamke alipoona, ya kuwa hakufichika, akaja na kutetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu ya kumgusa na jinsi alivyopona papo hapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mwanamuke alipoona kwamba ametambulikana, akakuja akitetemeka kwa woga na kujitupa mbele ya Yesu. Na pale mbele ya watu wote, akaeleza sababu gani alimugusa na namna alivyoponyeshwa mara moja.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yule mwanamke alipoona ya kuwa hakustirika, akaja akitetemeka, akamwangukia, akamweleza mbele ya watu wote sababu hatta akamgusa, na jinsi alivyoponywa marra moja.