Luke 8:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda hizo mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga na ndege wakazila.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia; zikakanyagwa, nao ndege wa angani wakazila.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Mkulima alikwenda kupanda mbegu. Alipokuwa akizitawanya, baadhi zilianguka kandokando ya njia. Watu wakazikanyaga, na ndege wa angani wakazila.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda zile mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga, na ndege wakazila.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda hizo mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga na ndege wakazila.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mpanzi alitoka kwenda kusia mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, zikakanyagwakanyagwa na ndege wa angani wakazila.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia; zikakanyagwa, nao ndege wa angani wakazila.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda hizo mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga na ndege wakazila.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mpanzi alitoka kuzimiaga mbegu zake. Ikawa, alipozimiaga, nyingine zikaangukia njiani, zikakanyagwa, nao ndege wa angani wakazila.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mupandaji mumoja alikwenda kupanda mbegu. Alipokuwa akipanda mbegu katika shamba lake, zimoja zikaanguka pembeni ya njia. Watu wakazikanyagakanyaga na ndege wakazikula.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda, nyingine zikaanguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege za anga wakazila.