Luke 8:51 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipofika nyumbani mwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, pamoja na baba na mama wa yule binti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akaenda nyumbani, alipofika akaruhusu Petro, Yohana, Yakobo pamoja na baba na mama wa yule mtoto tu kuingia ndani pamoja naye.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipofika nyumbani kwa Yairo, hakumruhusu mtu ye yote aingie ndani pamoja naye isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, baba na mama wa yule binti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipofika nyumbani kwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, pamoja na baba na mama wa yule binti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipofika nyumbani hakuruhusu mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipofika nyumbani hakumruhusu mtu kuingia ndani pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohane, Yakobo na wazazi wa huyo msichana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoingia nyumbani hakumpa mtu ruhusa kuingia pamoja naye, ila Petero na Yohana na Yakobo na baba yake mwana na mama yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipofika nyumbani hakuacha mtu kuingia pamoja naye ila Petro, na Yohana, na Yakobo, na babaye yule mtoto na mamaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipofika ndani ya nyumba ya Yairo, hakuruhusu mutu kuingia pamoja naye isipokuwa Petro, Yoane, Yakobo, baba na mama wa mutoto.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipofika nyumbani, hakumwacha mtu aingie pamoja nae, illa Petro, na Yakobo na Yohana, na baba yake yule kijana na mama yake. Na watu wote walikuwa wakilia, wakimwombolezea.