Luke 8:7 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mbegu zingine ziliangukia kwenye miiba. Miiba ikakua pamoja nazo, miiba ikazisongasonga na hazikukua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, ile miiba ikakua pamoja nazo na kusonga hiyo mimea ikafa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyingine zikaangukia miibani katikati, nayo miiba ikaota pamoja nazo, ikazisonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbegu zingine zikaanguka katikati ya miiba. Ile miiba ikaota pamoja na mbegu, na kuzisonga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nyingine zikaanguka kati ya miiba, nayo miiba ikamea pamoja nazo, ikazisonga.