Luke 9:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuponya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu aliwaita mitume wake kumi na wawili pamoja, akawapa nguvu kuponya magonjwa na kutoa pepo kwa watu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo juu ya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuponya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akiisha kuwaita wale kumi na wawili pamoja, aliwapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaita wale Kumi na Wawili, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliwaita wale kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuponya pepo wote, na uwezo wa kuponya wagonjwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaita wale kumi na wawili, wakusanyike, akawapa uwezo na nguvu za kufukuza pepo wote na za kuponya magonjwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawakusanya wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapatia uwezo na mamlaka ya kufukuza pepo, na uwezo wa kuponyesha wagonjwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi.