Luke 9:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini umati wa watu wakafahamu alikoenda, wakamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini watu walipotambua mahali alikokwenda Yesu walimfuata. Aliwakaribisha na kuwaambia kuhusu ufalme wa Mungu. Na aliwaponya waliokuwa wagonjwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini umati wa watu ulipofahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini umati wa watu ukafahamu alikokwenda, ukamfuata. Akawakaribisha na kunena nao kuhusu Ufalme wa Mwenyezi Mungu na kuwaponya wale wote waliokuwa wanahitaji uponyaji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wale watu walipojua alikokwenda, walimfuata. Yesu akawakaribisha akawazungumzia juu ya ufalme wa Mungu, akawaponya wale waliohitaji kuponywa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makundi ya watu walipovitambua wakamfuata, naye akawapokea, akasema nao mambo ya ufalme wa Mungu, akawaponya waliopaswa na kuponywa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini makundi ya watu walipopata habari ile, wakamufuata mpaka kule. Yesu akawapokea na kuanza kusema nao juu ya Ufalme wa Mungu, na vilevile akawaponyesha wale waliohitaji kuponyeshwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa.