Luke 9:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage watu hawa ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baadaye nyakati za jioni. Mitume kumi na mbili walimwendea na kumwambia, “Hakuna anayeishi mahali hapa. Waage watu. Wanahitaji kutafuta chakula na mahali pa kulala katika mashamba na miji iliyo karibu na eneo hili.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakamjia Yesu na kumwambia, “Uage umati huu wa watu uondoke ili uweze kwenda kwenye vijiji vya karibu na sehemu za jirani, ili kupata chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, “Waage makutano ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Kumi na Wawili, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jua lilipokuwa linaanza kutua, wale kumi na wawili walimwendea wakamwambia, “Waage watu waende kwenye vijiji na mashamba ya karibu, wakajipatie chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tulipo ni nyikani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jua lilipotaka kuchwa, wale kumi na wawili wakamjia, wakamwambia: Uliage kundi la watu, waende zao vijijini na mashambani huko pembenipembeni, waone ulalo na vyakula, kwani hapa tulipo ni nyika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jua lilipoanza kushuka, wanafunzi kumi na wawili wa Yesu wakamufikia na kumwambia: “Hapa tunapokuwa ni katika pori. Uage makundi haya ya watu kusudi waende katika vijiji vinavyokuwa hapa karibu na kwenye nyumba kule katika mbuga kwa kujitafutia chakula na nafasi ya kulala.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu.