Luke 9:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wote wakala, wakashiba. Wakakusanya mabaki ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wote wakala mpaka wakashiba. Vikasalia vikapu kumi na mbili vilivyojaa vipande vya mikate na samaki ambavyo havikuliwa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakala wote, wakashiba; wakakusanya makombo ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wote wakala, wakashiba. Wakakusanya mabaki ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyobaki, vikajaa vikapu kumi na viwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wote wakala, wakashiba. Wakakusanya mabaki ya chakula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakala, wakashiba wote, pakaokotwa makombo yaliyowasalia vikapu kumi na viwili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote wakakula na kushiba. Nao wanafunzi wakaokota vipande vilivyobaki, wakajaza vitunga kumi na viwili.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakala, wakashiba wote: na vile vipande vilivyowabakia vikaokotwa, vikapu thenashara.